Barua Njingine Ya Orange Football Academy Kwa Tff

 

7 Aug, 2013

Katibu Mkuu

 

TFF

Dar es salaam

Kutokana na Kanuni za TFF kipindi hiki ni kwa watu, vilabu vyenye kuona kuna utata, matatizo kuyaleta kwenu ili daftari la usajili liweze kushafishwa na kila mchezaji apate uhalali tayari kwa Ligi Kuu ya ijayo.

Klabu ya Oranje ya Zanzibar kwa mara nyengine tena inapenda kukuletea malalamiko kuwa mchezaji SEIF ABDULLAH (KARIHE)  hangepaswa toka msimu uliopita kuwemo katika orodha na kuchezea timu ya Azam, na bado hana uhalali akiendelea kuchezea Klabu hiyo ya Azam.

Hili ni lalamiko letu la tatu kwako kwa mchezaji huyo kwa vile mara ya kwanza tulileta mchezjai huyo alipojiunga na JKT Ruvu bila ya kufanyiwa uhamisho kutoka Oranje ya Zanzibar, kama vile mchezaji huyo alikuwa huru.

Kisha pia alipojiunga na Azam kutoka JKT Ruvu pia tulillamika nab ado TFF ikanyamaza kimya na kumhalalisha kwa Azam kwa hisia pengine ametoka JKT Ruvu wakati tulileta taarifa kwa maandishi kuwa si JKT Ruvu wala Azam waliomhamisha kilalali kutoka kwetu.

Lakini pia tunaleta lalamiko juu ya mchezaji MUDATHIR YAHYA ABBASS ambae pia amesajiliwa na Azam amekuwa mchezaji wetu halali na Azam hawakufanya uhanmisho wowote kutoka kwetu kama kwamba mchezaji huyo wamekuja kumchuma kwenye mti huku kwao Zanzibar.

Tunaomba TFF ichukue katika hili na itukutanishe na Azam ili tufikie suluhisho juu ya wachezaji hao.

Kwamba wamekuwa wachezaji wa Azam kwa zaidi ya msimu mmoja, kwa kila haki, haiwafanyi wawe ni halali kuchezea Azam, kwa sababu Klabu yetu haijapata haki yake kwa kuchukuliwa na timu hiyo

Ally Saleh

Oranje Football Academy

Email : This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

0777 430022/ 0715 430022