U17 Yatinga Hatua Ya Nne Bora,Yaichapa Sap-Soap 3-0

 

Orange Football Academy (O.F.A) U17 Leo Jumapili 02-06-2013 Wameendeleza Kasi Yao Ya Ushindi Baada Ya  Kutoa Kipigo Kitakatifu Kwa Vijana Wa Sap-Soap Cha Goli 3 - 0 Mchezo Uliochezwa Katika Kiwanja Cha Amani "B" Saa 4:00 Asubuhi.

Vijana Wa O.F.A Wakicheza Soka Safi Walipata Goli La Kwanza Dakika 35 Kupitia Mpira Wa Adhabu Uliokwenda Moja Kwa Moja Wavuni Adhabu Hio Ilichongwa Na Mchezaji Fahad Adam (Alaves), Goli La Pili Lilifungwa Na Mchezaji Omar Ramadhan (Masta) Dakika 63 Wakati Goli La Tatu Lilifungwa Na Mchezaji Abdulhalim Hafidh (Didie) Dakika Ya 68 Na Kuihakikishia  O.F.A Kutinga Hatua Ya Nne (4) Bora Za Kutafuta Bingwa Wa Ligi Ya Junior Msimu Wa 2013.

Nyota Hao Wa U17 Wameendeleza Wimbi La Ushindi  Kwa Timu Za Group "A" Baada Ya  Mchezo Wa Kwanza Wa Kundi Hilo Kutoka Sare 2 - 2, Walianza Kasi Yao Katika Mechi Ya Pili Kwa Ushindi Wa Mabao  2 - 0, Watatu 3 - 0 Na Mchezo Wa Nne 3 - 0. Hivyo Kufikisha Point 10 Na Magoli 10. Na Kuweza Kutinga Nne (4) Bora.
 
Katika Maandalizi Ya Nne (4) Bora Chipukizi Hao Wa U17 Kesho Wataanza Mazoezi Rasmi Kujiandaa Na Hatua Hio Ya Fainali  Za Kutafuta Ubingwa Huku Mwalimu Wao Hashim Ali Akifurahishwa Na Vijana Wake Baada Ya Kuonyesha Kiwango Kizuri Katika Hatua Zilizopita Na Pia Kuwataka Wachezaji Wote Kujituma Kwa Bidii Ili Kuweza Kupata Matokeo Mazuri Katika Hatua Hio Ya Mwisho Ya Fainali. 
 
Katika Pambano Jingine La Ligi Lililofanyika Jana Tarehe 01-06-2013 Orange Football Academy U17  Waliweza Kushinda Magoli 3 - 0 Baada Ya Kufunga Timu Ya New Znz Academy, Magoli Yote Yakifungwa Na Mchezaji Hatari Fahmi Agogo Katika Dakika Ya 5 Kipindi Cha Kwanza, Dakika Ya 56 Kipindi Cha Pili Na Dakika 63.

Kutokana Na Mchezo Mbaya Nyota Huyo Baadae Alijikuta Akitolewa Nje Na Muamuzi Kutoka Na Kumchezea Rafu Mchezaji Wa Timu Ya New Znz Academy.

Hata Hivyo Kikosi Hicho Cha U17 Kilijikuta Kikipoteza Nafasi Nyingi Zilizotengeneza Na "Star" Ujudi Ambaye Aliweza Kumiliki Nafasi Ya Kiungo Kwa Vizuri Hivyo Kutokana Na Kutozitumia Nafasi Hizo Kulipunguza Kasi Ya Vijana Hao Kutoka Uwanjani Na Ushindi Mnono Zaidi.