Oranje Football Academy Yafunga Mazoezi Kuupisha Mfungo Wa Ramadhani

Kituo cha orange football  Academy kimefunga rasmi mazoezi hadi baada ya kumaliza mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan na sikukuu yake,
 
lakini katika jitihada zake za kukuza na kuendeleza soka la vijana nchini kituo kimeamua pia kubadilisha mfumo wa kukusanya na kuviendeleza vipaji vya vijana kwa sasa kuamua kuwakusanya watoto wa mitaani wanaopenda soka na kuwaanzishia mashindano yao kwa lengo la kuviendeleza vipaji VINAVYOZURURA MITAANI NA KUWASHAJIISHA KUSOMA SKULI NA VYUONI KWA LENGO LA MAISHA YAO YA BAADAE NA KUJA KUWA WACHEZAJI BORA.
 
Katika mpango huo kituo kimeanza kwa mechi za kawaida wiki iliyopita ambapo wiki hii tunakusudia kuwa na bonanza maalum na tutakuja kuendelea na mipango hii rasmi baada ya mwezi mtukufu wa ramadhani.
 
Pichani  ni  vijana hao wakiwa katika mechi wiki iliyopita  katkika moja ya viwanja vya orange football academy (ofa).