Bonanza Yaendelea Kushika Kasi

 

Kituo cha kukuza vipaji vya soka kwa vijana nchini Orange Football Academy kinaendelea vizuri na utafutaji wa vipaji kutoka katika vijana wa mitaani ambao hawana vilabu ambao wana uwezo mkubwa kisoka (pichani) ni matukio ya bonanza la majaribio lililofanyika mwisho wa wiki iliyopita chini ya usimamizi wa mwalimu mahiri wa watoto Hashim (Kibabu) na baada ya bonanza hilo vijana kupatiwa zawadi mbali mbali ikiwamo vifaa vya kusomea na mipira.

 

Tayari kituo kimeamua kuwa na utaratibu huo na uwe nelevu kwa watoto wa mitaani.

 

Tunawaomba makocha na viongozi wa vilabu vyote vidogo kujitokeza katika Bonanza hio ili kujipatia wachezaji wenye vipaji kwaajili ya vilabu vyao pamoja na kuwaendeleza vijana hao kisoka na kimasoma badala ya kuwawacha kuzurura mitaani.

Tunawaomba pia wale wote watakuwa na mchango wowote wa kusaidia mpango wetu huu tunawakaribisha kwa msaada wowote ule,kama ni wa vifaa vya michezo,masomo,dawa au fedha zitakazosaidia kuendelea kuwasaidia vijana hao ambao ndio taifa la baadae.